Wakiwa wamebeba bendera za utawala wa Kizayuni na ile ya utawala wa zamani wa wa ufalme wa kidikteta Iran, wahalifu hao waliharibu sehemu ya jengo la kituo hicho. Kwa mujibu wa taarifa, walikuwa miongoni mwa makundi yanayopinga mapinduzi, na kitendo chao kinaonekana kama sehemu ya njama zinazodaiwa kupangwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Polisi wamesema kuwa watu 14 kutoka katika kundi hilo wamekamatwa kwa kosa la kuvuruga utulivu wa umma.
Tukio hili linajiri wakati ambapo chuki dhidi ya Iran yaani Iranophobia na chuki dhidi ya Uislamu yaani Islamophobia zimekuwa zikiongezeka kwa kasi katika nchi za Magharibi, hali inayochochea mazingira ya uhasama dhidi ya jamii za Kiislamu.
Wakati huohuo, Iran imerejea katika hali ya utulivu baada ya kukabiliana na machafuko ya karibuni, na wananchi kurejea katika shughuli zao za kawaida katika miji mbalimbali. Hali hii imewakasirisha makundi ya uchochezi yanayotaka vurugu ziendelee.
Mapema mwezi huu, waandamanaji wenye misimamo mikali wanaodaiwa kuungwa mkono na utawala wa Kizayuni na Marekani waliharibu mali za umma na binafsi katika miji kadhaa nchini Iran, na kusababisha vifo vya raia na maafisa wa usalama, pamoja na kuwajeruhi wengine.
Walivunja miundombinu ya umma, wakafunga barabara, kushambulia majengo ya serikali na vituo vya polisi, na kuua au kujeruhi maafisa wa usalama. Aidha, walichoma moto misikiti kadhaa na kukivunjia heshima Kitabu Kitukufu cha Qur’ani.
Baadaye, maandamano makubwa yalifanyika kote Iran kulaani vitendo vya waandamanaji hao na wale wanaodaiwa kuwaunga mkono—Marekani na utawala wa Kizayuni.
Your Comment